Chagua habari kuu za mwaka 2015

12 votes
1. Msukosuko wa wakimbizi uliotokana na mgogoro wa mashariki ya kati. Watu zaidi ya 3000 walikufa maji wakijaribu kuingia Ulaya kwa njia ya bahari.
 
8% / 1 vote
2. Shambulizi la kigaidi katika chuo Kikuu cha Garrisa nchini Kenya lilisababisha vifo vya watu 147, wengi wao wakiwa ni wanafunzi.
 
17% / 2 votes
3. Kuibuka kwa kundi la ISIS na kuwa tishio kubwa kwenye eneo la mashariki ya kati, hasa baada ya kuonesha video za kutisha za mauaji ya kikatili.
 
0% / 0 votes
4. Mkutano wa pili wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika mjini Johannesburg, China ilitangaza kutoa dola za kimarekani bilioni 60 kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano na nchi za Afrika.
 
17% / 2 votes
5. Mkutano mkubwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa uliofanyika mjini Paris Ufaransa. Baada ya mazungumzo ya muda mrefu nchi zinazoendelea zimefanikiwa kuzibana nchi zilizoendelea kutoa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
 
8% / 1 vote
6. Kufikiwa kwa makubaliano ya suala la nyuklia la Iran, baada ya mazungumzo marefu. Nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na Ujerumani, zilifikia makubaliano na Iran, licha ya upinzani kutoka kwa waziri mkuu wa Israel na baadhi ya maseneta wa Marekani.
 
0% / 0 votes
7. China yachukua hatua za kihimiza ujenzi wa uhusiano mpya wa kimataifa. Uhusiano ambao lengo lake ni pande mbili kuheshimiana na kunufaishana, tofauti na utaratibu ambao unazikandamiza na kuzinyonya na kuzikandamiza nchi ndogo.
 
8% / 1 vote
8. Mwaka huu kulikuwa na chaguzi nyingi za urais, lakini matokeo ya chaguzi za Tanzania na Nigeria ndio yamevutia, hasa baada ya washindi kuonesha kuleta aina mpya ya utendaji kazi. Rais John Magufuli wa Tanzania kupunguza na matumizi ya serikali, na Rais Muhamadu Buhari kuonesha nguvu kupambana na ufisadi na kundi la Boko Haram.
 
25% / 3 votes
9. Kulikuwa na jaribio la mapinduzi nchini Burundi wakati Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza akihudhuria mkutano wa jumuiya ya Afrika mashariki nchini Tanzania, baadaye kulitokea mvutano wa kuhusu kama kugombea kwake urais, baada ya kugombea na kushinda, maandamano ya kumpinga yalisababisha vurugu.
 
0% / 0 votes
10. Tetemeko kubwa la ardhi chini Nepal lililosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 9.
 
17% / 2 votes


Click here to share poll on specific pages, user profiles or purchase votes!